DPP awafutia kesi Mashehe wa Uhamsho na Bosi wa IPTL Harbinder Seth

Na Rebecca Kwandu, Kisutu

Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Sylivester Mwakitalu amewafutia mashtaka watuhumiwa 36 wa makosa ya ugaidi baada ya ushahidi kuwa hafifu na Mmiliki wa Kampuni ya Kufufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth baada ya kukiri kosa na kuilipa fidia serikali ya kiasi cha shilingi bilioni 26.9.
Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Sylivester Mwakitalu.

Kesi ya Harbinder Seth iliongozwa na Mawakili wa Mashtaka Marteus Marandu,Renatus Mkunde, Wankyo Simon na Faraja Ngukah ambapo wakili wa utetezi alikuwa Melchizedek Lutema ambaye alikubaliana na maelezo yaliyotolewa na Mawakili wa Mashtaka yaliyoainisha kuwa mshtakiwa Harbinder Seth alikuwa anakabiliwa na mashtaka kumi yakiwemo ya kughushi nyaraka,kutakatisha fedha na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo baada ya kufanyika majadiliano kati ya DPP na Seth, mshitakiwa alipunguziwa Mashtaka na.kubakiwa na shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu ya Seth ilitolewa jana Juni,2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Mhe. Huruma Shahidi ambapo Juni 10,2021 Harbinder Seth aliandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtakau kuomba kukiri Mashtaka yake na kupunguziwa adhabu.

Wakati huo huo viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar wamefutiwa Mashtaka na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylivester Mwakitalu kutokana na kuwepo kwa udhaifu wa ushahidi.

Kesi hiyo ilichelewa kusikilizwa kutokana na ushahidi kuchelewa kukamilika.Uamuzi wa DPP unafuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ambapo Mahakama Kuu ilishawafutia Mashtaka 14 na Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa ya DPP kwa kueleza kuwa ushahidi uliowakilishwa ulikuwa dhaifu na usiotosha kuwatia hatiani washtakiwa.

"Kwa upande wetu tumefikia hatua ya kuondoa mashtaka yote. Mamlaka ya Zanzibar zikiona inafaa zitaendelea nao,"amesema DPP Mwakitalu.

Post a Comment

0 Comments