Katavi yaitambia Dar mpira wa wavu

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Timu ya mpira wa wavu ya wasichana kutoka mkoa wa Katavi jana iliifunga timu ngumu kutoka Dar es salaam kwa seti 3-1 katika mchezo wa kusisimua uliochezwa katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara.
Timu hiyo ya katavi ambayo ilitolewa hatua ya nusu fainali katika mashindano ya mwaka 2019 ilionyesha ushindani wa hali ya juu kwa Dar es salaam ambao ndiyo mabingwa watetezi wa kombe hilo kwa wasichana.

Matokeo mengine katika michezo hiyo ambayo ipo katika hatua ya makundi kwa wasichana inaonyesha kuwa Manyara iliifunga Dodoma seti 3-0, Mbeya iliichapa Simiyu kwa seti 3-0, wenyeji Mtwara wameifunga Tabora kwa seti 3-0, Ruvuma wamefungwa na Tanga kwa seti -0, Singida wameifunga Kagera seti 3-0, Manyara wameifunga Dodoma seti 3-0, na Iringa wameifunga Lindi kwa seti 3-1.

Matokeo ya mpira wa wavu kwa wavulana yanaonyesha Tabora wameifunga Songwe seti 3-0, Mbeya wameifunga Simiyu seti 3-0 na Geita wamefungwa, Tabora kwa seti 3-1, Dar es salaam wameifunga Mwanza seti 3-1, Pwani imeichapa Mara seti 3-1, Manyara imeifunga Simiyu seti 3-1 na Lindi imeifunga Iringa seti 3-1.

Kwa upande wa mpira wa miguu matokeo kwa wavulana yanaonyesha Geita 3 Lindi 1, Dar es salaam 3 Pwani 0, Kigoma 4 Njombe 0.

Matokeo ya mpira wa miguu kwa wavulana yaani soka maalum yanaonyesha Geita 0 Njombe 2, Kigoma 1 Mwanza 0, Rukwa 0 Mtwara 1, Ruvuma 1 Dar es salaam 0.

Kwa upande wa matokeo ya mpira wa miguu wasichana Kagera 1 Simiyu0, Iringa 0 Manyara 5, Geita 1 Katavi 0, Tabora 1 Arusha 0, Mara 1 Dar es salaam 2, na Rukwa 1 Dodoma 0.
Matokeo ya mpira wa mikono kwa wavulana yanaonyesha kuwa Tanga imefunga magoli 12 dhidi ya 6 ya Shinyanga, huku Kigoma 5 mwanza 14, Arusha 18 Ruvuma 19, Morogoro 12 Tabora 14, Ruvuma 6 Songwe 14, Iringa 7 Dar es salaam 23, Singida 21 katavi 11, Simiyu 9 Njombe 9, Kilimanjaro 14 Mwanza 18 na Morogoro 27 Arusha 10.

Kwa upande wa wasichana matokeo ya mpira wa mikono Rukwa 5 Mtwara 11, Lindi 12 Dodoma 9, Kilimanjaro 2 Manyara 6, Mbeya 9 Simiyu 9, Njombe 1 Morogoro 26, Dar es salaam 16 Mtwara 17, Rukwa 2 Songwe 7, Tanga 26 Shinyanga 15.

Matokeo ya mpira wa goli kwa michezo iliyomalizika jana jioni kwa upande wa wavulana yanaonyesha Mtwara 9 Rukwa 9, Iringa 16 Kigoma 4, Mara 8 Mtwara 10, Tabora 3 Njombe3, Dodoma 24 Pwani 4, Rukwa 12 Katavi 7, Geita 5 Shinyanga 16

Matokeo ya mpira wa goli kwa wasichana Tanga imefungwa na Mbeya kwa magoli 12-3.

Kwa upande wa mpira wa Netiboli matokeo yanaonyesha Shinyanga imefungwa na Tanga kwa magoli 33-9, Songwe imeifunga Simiyu magoli 29-9, Iringa imefungwa na Kilimanjaro kwa magoli 11-13, Geita imeifunga Katavi 30-3, Dar es salaam na Mbeya zimetoka sare kwa kufungana magoli 24-24 na Arusha imefungwa na Dodoma kwa magoli 20-19.

Post a Comment

0 Comments