KMC FC KUWAKABILI DODOMA JIJI KESHO UWANJA WA JAMHURI

Kikosi cha KMC FC hapo kesho kitashuka katika Dimba la Jamuhuri Jijini Dodoma kuwakabili Timu ya Dodoma Jiji,mchezo ukaopigwa saa 16:00 jioni huku Kocha msaidizi wa Timu hiyo Habibu Kondo akisema wamejipanga vizuri kuhakikisha kwamba wanaondoka na alamatatu muhimu.
Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dodoma, Habibu amesema kuwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu lakini bado upondani ya uwezo wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni na kwamba maandalizi yamefanyika kwa asilimia kubwa.

Ameongeza kuwa,KMC FC inaiheshimu Dodoma Jiji kutokana na ubora waliokuwa nao hasa wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani lakini akasisitiza kuwa maandalizi yaliyofanyika yamelenga kusawazisha makosa mbalimbali na hivyo kupata matokeo mazuri ugenini hapo kesho.

“Mchezo wa kesho unaumuhimu mkubwa kutokana na kwamba Ligi imegawanyika katika makundi matatu hadi sasa ambayo ni kupambania kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu, kuendelea kusalia kubaki ligi Kuu lakini pia kumaliza katika nafasi ya Nne jambo ambalo KMC FC tupo kwenye kundi la kuwania nafasi hiyo ya Nne ambayo kimsingi ipo ndani ya uwezo wetu,” amesema Kocha Habibu.

Habibu amesema katika mchezo wa kesho watakosekana wachezaji muhimu wa Nne ambao Hassan Kabunda, Charles Ilamfya, David Brayson pamoja na Abdul Hillary kutokana na sababu za kuwa na majeraha na kwamba wachezaji wengine wapo kwenye ubora mkubwa ambao licha ya kukosekana kwa nyota hao lakini KMC FC imejizatiti kupata matokeo mazuri.

Kwa upande wake Nahodha wa KMC FC, Juma Kaseja amesema kuwa anaamini katika mchezo wakesho ambaye amejipanga vizuri atapata matokeo na kikubwa ni kumuomba mungu Timu zote mbili kuanzia leo hadi kesho washinde na walale salama ili kila mmoja akatimize majukumu yake uwanjani.
Imetolewa leo Juni 16

Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa KMC FC

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news