KMKM SC yatwaa ubingwa Ligi Kuu Zanzibar

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Timu ya KMKM SC imeweka rekodi sawa na Mlandege FC na kuwa Mabingwa wa Kihistoria kwenye Ligi Kuu Soka ya Zanzibar.

Timu hizo za KMKM na Mlandege ndio wanaongoza kubeba vikombe katika Ligi Kuu Soka ya Zanzibar mara saba wakifuatiwa na Small Simba wanaoshika nafasi ya 3tatukwa kutwaa kombe hilo mara tano.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar Timu ya KMKM Zanzibar wakishangilia Ubingwa wao baada ya kukabidhiwa Kombe wa Ubingwa kwa msimu wa mwaka 2021 /2022, kwa kuibuka Bingwa wa Ligi hiyo kwa kumaliza mchezo wao wa mwisho kwa ushindi uliofanyika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
HISTORIA YA USHINDI IPO HIVI;

KMKM wameshinda mara saba
1984
1986
2004
2012-2013
2013-2014
2018-2019
2020-2021

Mlandege wameshinda mara saba
1996
1997
1998
1999
2001
2002
2019-2020

Small Simba wameshinda mara tano
1983
1985
1988
1991
1995

Post a Comment

0 Comments