Tanzania yaichapa Malawi 2-0 dimba la Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Timu ya Tanzania ya Taifa Stars imetumia vizuri dimba la nyumbani la Benjamin Mkapa leo Juni 13, 2021 lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salam kwa kuwarejesha nyumbani wageni wao kwa mabao mawili.
Wageni hao walikuwa ni Timu ya Taifa ya Malawi ambao wameadhibiwa magoli hayo katika mchezo huo wa kirafiki ukiwa katika kalenda ya michezo ya Kimataifa ya shirikisho la mpira Duniani (FIFA).

Mtanange huo mzuri, ulionekana mgumu kwa kipindi cha kwanza ambapo si Tanzania wala Malawi waliweza kupata magoli.

Aidha, dakika ya 68, nahodha John Bocco alizitikisa nyavu za The Flames ambalo lilidumu dakika chache huku Israel Patrick Mwenda akifunga bao lingine.

Mwenda alifunga bao hilo ndani ya dakika ya 75 kwa usaidizi mzuri wa nyota wa Mbeya City, Kibu Dennis.

Dennis aliyetokea benchi kipindi cha pili akiwa na ari kubwa ambapo alianza kumtengenezea John Bocco kabla ya kuangushwa nje kidogo ya boksi na Mwenda akafunga kwa shuti la mpira wa adhabu.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kilichocheza na Malawi;

Post a Comment

0 Comments