Mwenyekiti Jaji mstaafu Steven Bwana kuongoza Mkutano wa Nne wa Tume ya Utumishi wa Umma kuanzia leo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, ataongoza mkutano wa Nne wa Tume kwa mwaka wa fedha 2020/2021 unaofanyika, Jijini Dar es Salaam, kuanzia leo Jumatatu tarehe 21 Juni hadi tarehe 02 Julai 2021.
Katika Mkutano huu Tume itapokea na kutolea uamuzi Rufaa 107 na Malalamiko 06 yaliyowasilishwa na Watumishi mbalimbali wa Umma, ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka zao za Nidhamu.

Shughuli nyingine iliyopangwa kufanyika katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili:-

Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma katika kipindi cha Robo ya Tatu (Januari hadi Machi ) ya mwaka wa fedha 2020/2021.

Tume ya Utumishi wa Umma inatekeleza majukumu haya kwa mujibu wa Kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 (Marejeo ya mwaka 2019).

Post a Comment

0 Comments