Rais mstaafu Dkt.Kenneth David Kaunda afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Kwanza wa Zambia, Dkt. Kenneth David Kaunda amefariki dunia leo Juni 17,2021 akiwa na miaka 97.
Kaunda anafahamika zaidi kama KK amezaliwa Aprili 28, 1924.

Siku chache zilizopita, Dkt. Kaunda alilazwa katika Hospitali ya Maina Soko jijini Lusaka kufuatia maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa siku kadhaa.

Dkt.Kaunda aliitawala Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1991

Post a Comment

0 Comments