RAIS SAMIA AZINDUA MITAMBO MIPYA YA KISASA YA MATIBABU YA MOYO CATHLAB NA CARTO 3 SYSTEM TAASISI YA JKCI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI, Dar

Leo Juni 12, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amezindua mtambo mpya wa matibabu ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo katika hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.

Mtambo huo unaifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa nchi pekee inayotoa matibabu ya hali ya juu ya kibingwa Afrika Mashariki na Kati.

Aidha, mtambo huo wenye uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 System 3D&mapping electrophysiology System una uwezo wa kufanya uchunguzi na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee ma Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kuzindua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo katika hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mitambo mipya ya uchunguzi na tiba ya maradhi ya moyo ‘Catheterization laboratory na Carto 3, Rais Samia amesema kwamba mitambo hiyo itaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nane Afrika zenye mitambo ya aina hiyo.

“Mitambo ya Cathelab na Carto 3 tunayo zindua leo ni ya kisasa zaidi na imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.6 . Mitambo hii itatufanya tuwe miongoni mwa nchi nane Afrika yenye mitambo ya aina hiyo, Tanzania kwa sasa tunakwenda juu katika utambuzi na tiba za maradhi ya moyo,"amesema Rais Samia.

Mhe.Rais Samia amesema kwamba, Taasisi ya JKCI imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania na wasio Wantaaznia kwani mpaka sasa wagonjwa wapatao 5,959 wamepatiwa matibabu ya upasuaji wa moyo ambapo kati yao wagonjwa 11 sawa na asilimia 0.2 walipoteza maisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI mara alipotembelea chumba cha Wodi ya Watoto wenye uhitaji wa Uangalizi maalum kabla ya kuzindua mitambo ya Catheterization Laboratory pamoja na Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system katika Taasisi hiyo.

Akizungumzia magonjwa yasiyoambukiza , Rais Samia anasema kwamba magonjwa hayo kama vile moyo, kisukari, figo na saratani yanaongezeka duniani kote ikiwemo Tanzania ambapo ongezeko hilo linachangiwa pia na kukuwa kwa wataalam wa kugundua magonjwa hayo kwani kabla ya wataalam nchini kuwepo wagonjwa wengi walipoteza maisha pasipo kufahamu nini chanzo cha tatizo.

Takwimu za magonjwa yasiyoambukiza duniai zinaonyesha kwamba mwaka 2016 kulitokea vifo milioni 41 sawa na asilimia 71 ya vifo vyote wakati huo ambapo kwa Tanzania asilimia 33 ya vifo vilitokana na magonjwa yasiyoambukiza huku moyo na shinikizo la damu vikisababisha vifo kwa asilimia 13

"Asilimia 13 ya vifo kutokana na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu ni kiasi kikubwa sana kuacha itokee nchini, kwa kuzingatia hilo leo tuna furaha kubwa kuzindua mitambo hii ya tiba na uchunguzi wa moyo, lengo ni kupunguza asilimia hizo za vifo,"amesema.

Pamoja na kuahidi kushughulikia changamoto zinazonaikabili taasisi hiyo ikiwepo upungufu wa watumishi na punguzo la msamaha wa matibabu, Rais Samia pia amepongeza watumishi wa taasisi hiyo kwa kazi yao ya kipekee na yenye kuhitaji utaalamu wa aina yake, “Kazi mnayoifanya sijui niipe sifa gani, maana naogopa kukufuru, lakini kuweza kusimamisha moyo wa mwanadamu kwa saa kadhaa, sio kazi ya kawaida,”amesema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi alipokuwa akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hiyo kabla ya uzinduzi wa mitambo hiyo ya Kisasa.Amesema mtambo huo umenunuliwa na Serikali kwa thamani ya Sh4.6 bilioni fedha zilizotolewa mwaka jana mwanzoni.

Naye Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema kwamba hospitali zote za rufaa ikiwemo JKCI zipo kwenye mchakato wa kuandaa maandiko ili kuweza kupata ithibati ya kimataifa lengo ni kutengeneza utalii wa kitabibu hapa nchini.

“Tupo kwenye maboresho katika hospitali zetu zote za rufaa, tumekubaliana baada ya kupata mitambo ya kisasa sasa tuandae maandiko na kufuata taratibu zote ili tuweze kupata ithibati ya kimataifa, lengo letu kubwa ni kuifanya Tanzania kuwa kituo cha utalii katika kada hii ya afya. Hospitali zetu zote kama vile Ocean Road, MOI, Benjamini Mkapa na nyingine zinakimbizana kukamilisha jambo hilo,"amesema Dkt. Gwajima.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi wakati akitoka kutembelea Wodi ya Watoto katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohammed Janabi amesema kazi zitakazofanywa na mtambo mpya wa kisasa wa kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo ni kuchunguza mishipa ya damu ya moyo.

Ametaja kazi nyingine kuwa ni kuweka vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba na kutibu mfumo wa umeme wa moyo.

Mtambo huo wa kisasa zaidi ya Cathlab wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuchunguza na kutibu tatizo la hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo, ulianza kufanya matibabu kwa mgonjwa wa kwanza Aprili 30, 2021.

“Tunaishukuru Serikali kuiwezesha JKCI, kufunga mtambo huu wa kisasa, ni teknolojia ya hali ya juu, tutaweza kuokoa maisha ya watu wengi wenye matatizo ya moyo ikiwemo mfumo wa umeme wa moyo kupitia mashine hii,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo pamoja na kukagua mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Pia Profesa Janabi amesema, kwa kipindi kirefu wagonjwa wengi walikuwa wakienda kutibiwa nje ya nchi na baadhi yao walitibiwa nchini na kwamba mtu anaweza kuzaliwa na tatizo hilo au kulipata ukubwani kutokana na athari ya ugonjwa unaoweza kusababisha mfumo wa umeme wa moyo kubadili mapigo yake.

"Mara nyingi kuwa chini ya 60 kwa dakika na hivyo kusababisha mapigo kuwa chini sana au kuwa juu ya 100 kwa dakika na hivyo kuufanya moyo udunde kwa haraka, kawaida mapigo ya moyo huwa ni 60 hadi 100 kwa dakika,” amesema Profesa Janabi.

Amesema, utaalamu zaidi wanaendelea kupata kutoka kwa mataifa mengine walioendelea, hivyo mtambo huo utakuwa mkombozi kwa wagonjwa wengi.

“Tanzania ina wataalamu wa kutosha, tumewasomesha China na Afrika Kusini, kupitia kambi mbalimbali za matibabu ya moyo tunazofanya kwa kushirikiana na wenzetu wa nje ya nchi wenye utaalamu mkubwa zaidi yetu, tunajifunza utaalamu wa kutosha na wa kisasa; 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete pamoja na wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mtambo wa Kisasa Catheterization Laboratory uliounganishwa na mtambo wa Carto 3 system 3D and mapping electrophysiology system wenye uwezo wa kufanya uchunguzi, kufunga vifaa visaidizi vya moyo, kuzibua mishipa ya damu ya moyo na kutibu hitilafu ya mfumo wa umeme wa moyo. (Picha zote na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news