TAASISI YA UONGOZI KUTOA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO KIUTENDAJI VIONGOZI WOTE KUANZIA WIKI IJAYO

Na James K. Mwanamyoto, Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema, Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) imeandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo kiutendaji Viongozi wa Kisiasa na Viongozi Watendaji katika Utumishi wa Umma yatakayotolewa kuanzia wiki ijayo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anayetaka viongozi kutoa mchango wenye tija kwa maendeleo ya taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mchengerwa amesema hayo Juni 18, 2021 mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya UONGOZI katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, wajumbe wa bodi hiyo waliteuliwa hivi karibuni na Mheshimiwa Rais.

Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa, miongoni mwa viongozi watakaopatiwa mafunzo ni Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakurugezi wa Idara katika Taasisi za Umma.

Ameongea kuwa, mafunzo hayo elekezi yatakayotolewa yatawaandaa viongozi hao kutambua majukumu yao na kutekeleza kikamilifu wajibu wao, kwa mujibu wa Viapo vya Ahadi ya Uadilifu katika Utumishi wa Umma walivyovitoa.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Bw. Kadari Singo akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) kabla ya waziri huyo kuzindua Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI uliofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mchengerwa amesema, ukienda katika mataifa mengine ya Afrika Taasisi ya UONGOZI inasifika kwa kuwaandaa viongozi mbalimbali na imekuwa ni tegemezi katika kujenga uwezo wa viongozi barani Afrika, hivyo Serikali imeona ni vema taasisi hii itumike ipasavyo kutoa mafunzo kwa viongozi nchini ili waweze kuzingatia Miiko ya Uongozi na Maadili ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amewakumbusha viongozi wote kuwa, cheo ni dhamana hivyo kila kiongozi anaowajibu wa kuhakikisha anakitumia cheo chake kwa uadilifu mkubwa na kwa masilahi ya taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI wakionyesha vitendea kazi alivyowakabidhi kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa majukumu yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI, Dkt. Stergomena Tax akitoa shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa mara baada ya Waziri huyo kuzindua bodi hiyo leo katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Viongozi tambueni uongozi ni dhamana hivyo mnapaswa kuongeza ufanisi kiutendaji kwa kushiriki mafunzo yatakayotolewa na Taasisi ya UONGOZI hivi karibuni” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amesema Serikali inatarajia kuwa, baada ya viongozi kupata mafunzo haya ya kuwajengea uwezo, hakutakuwa na kiongozi yeyote atakayekwenda kinyume na Kanuni za Maadili ya Utendaji kazi katika Utumishi wa Umma za mwaka 2005.

Mara baada ya Mhe. Mchengerwa kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya UONGOZI, Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Stergomena Tax amemshukuru Mhe. Rais kwa kumteua yeye pamoja na wajumbe wengine wa bodi hiyo na kuahidi kuwa, watahakikisha wanatekeleza jukumu kubwa la Taasisi ya UONGOZI la kuwajenga viongozi ambao wataleta maendeleo endelevu katika taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI na watumishi wa taasisi hiyo mara baada ya kuzindua bodi hiyo katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Dkt. Tax amesema, wao kama bodi wanatambua umuhimu wa kuwa na viongozi mahiri wenye uwezo wa kuiwezesha nchi kupata maendeleo katika sekta mbalimbali nchini, hivyo watatekeleza wajibu wao kikamilifu kwa kutumia uwezo na uzoefu walionao.

Bodi ya Wakurugenzi Taasisi ya UONGOZI iliyozinduliwa leo inaundwa na Mwenyekiti Dkt. Stergomena Tax, Makamu Mwenyekiti Dkt. Laurean Ndumbaro na wajumbe wengine ni Prof. Penina Mlama, Prof. Samuel Wangwe, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mhe. Ritta Swan, Bi. Susan Mlawi, Bi. Lina Soiri na Bw. David Walker.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news