UEFA EURO 2020: England, Scotland zatoshana nguvu, Sweden yailaza Slovakia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Timu ya taifa ya England imelazimishwa sare ya bila kufungana na Scotland katika mchezo wa Kundi D usiku wa Juni 18, 2021 katika dimba la Wembley mjini London nchini Uingereza.

Mlinda mlango wa England, Jordan Pickford akiokoa kazi nzuri ya nyota wa Scotland, Stephen O’Donnell katika mtanange huo ndani ya dimba la Wembley. (Picha na Tom Jenkins/The Guardian/Diramakini Blog).Mameneja wamesema nini?

Bosi wa England Gareth Southgate anasema; "Ni matokeo ya haki, hatukufanya vema kushinda mchezo huu, au kutengeneza nfasi nyingi za kutuwezesha kuushinda, lakini pia hatukupaswa kupoteza. Nichukue nafasi hii kuwapongeza sana ndugu zetu wa Scotlabd, wamecheza vizuri na wameweza kujilinda vilivyo, hatukupata suluhu.

"Tulikuwa na nafasi nzuri, lakini hatukuweza kuitumia, mwishoni hatukuweza kufanya vizuri, lakini haya ni mashindano, tunajipanga, ingawa ni changamoto pale unapokosa ushindi,"amebainisha Southgate kama alivyokaririwa na DIRAMAKINI Blog.

Bosi wa Scotland Steve Clarke: "Stephen O'Donnell alikuwa wa kipekee sana na Billy alikuwa nyuma yake.Ilikuwa ni jambo jema sana kwake, kupata fursa ya kwanza ya kuanza ameutumia vema uwanja, mchezaji mkubwa, Billy. Nilikwisha sema kwa muda mrefu, huyu atakuja kuwa tegemeo kubwa sana siku za usoni katika mpira wa miguu kwa Uskochi, tunajua tutakachofanya huko kambini, tutaendelea kumuongoza zaidi ili aweze kufanya maajabu,"amebainisha.

Aidha, mechi nyingine ya kundi hilo, Croatia imetoa sare ya 1-1 na Jamhuri ya Czech Uwanja wa Hampden Park mjini Glasgow.

Kwa Sasa Czech na England kila moja ina pointi tatu baada ya mechi mbili kwanza, wakati Scotland na Croatia kila moja ina pointi moja.

Hata hivyo, katika mchezo wa Kundi E, Sweden imeshinda 1-0 dhidi ya Slovakia Uwanja wa Saint-Petersburg mjini Saint-Petersburg.

Post a Comment

0 Comments