Wanandoa wajilipua kwa Petroli kisa wazazi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wakazi wa Kijiji cha Busongo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Wenslausi James (30) na mkewe, Betha Kasimili (25) wamejilipua moto kwa kutumia mafuta ya Petroli, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wazazi wa James kumkataa mke wake.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Jackson Mwakagonda amewaambia waandishi wa habari leo Juni 16,2021 kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

Amesema, tukio hilo limetokea Juni 14, 2021 saa 4 asabuhi, katika kijiji cha Busongo Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu nyumbani kwao na mwanamke.

Ameongeza kuwa, wanandoa hao walikuwa wamejaliwa kupata watoto watatu, lakini wazazi wa mwanaume walimkataa mkwe wao na kuamua kuuvunja mji pamoja na kurudisha mahari nyumbani kwa mwanamke.

Post a Comment

0 Comments