Waziri Prof. Mkumbo ateua Wajumbe wa Bodi ya Uongozi Chuo cha Biashara (CBE)

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Eleuther Alphone Mwangeni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuanzia Juni 8, 2021. 

Prof. Mwangeni ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na anachukua nafasi ya Prof. Esther Ishengoma ambaye amemaliza muda wake.

Kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo , ameteua wajumbe sita (6) wa Bodi hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Chuo cha Elimu ya Biashara ya mwaka 1965 Sura 315 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2020.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.

Uteuzi wa Wajumbe hao utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 09, Juni, 2021. Wajumbe walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

1. Dkt. Consolatha Deogratias Ishebabi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo, Wizara ya Viwanda na Biashara;

2. Dkt. Kenneth Hosea ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;

3. Bi. Mwema Punzi ambaye ni Wakili wa Serikali Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;

4. Bw. Zahoro Muhaji ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF);

5. CPA. Peter Lucas Mwambuja ambaye ni Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA);

6. Waziri amemteua Prof. Wineaster Saria Anderson ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mjumbe wa Bodi ya CBE.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news