Waziri Ummy amsimamisha kazi Mhandisi wa Kinondoni, ujenzi Mwenge


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mheshimiwa Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Isack Mpaki.

Sambamba na kusimamisha ujenzi wa stendi ya mabasi Mwenge mkoani Dar es Salaam kupisha uchunguzi kutokana na kutoridhishwa na maendeleo ya mradi huo. 

Uamuzi huo ameuchukua baada ya kufanya ziara kwenye mradi huo leo Jumapili Juni 20, 2021.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy Mwalimu ameagiza wakuu wa mikoa kuwaapisha wakuu wa wilaya wote walioteuliwa kuanzia kesho Jumatatu Juni 21, 2021.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Jumapili Juni 20, 2021 muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake yake ya kukagua ujenzi wa stendi ya mabasi ya Mwenge.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy Mwalimu ameagiza wakuu wa mikoa kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa kuanzia kesho Jumatatu Juni 21, 2021.

“Kesho Jumatatu wote waanze mchakato wa kuwaapisha Wakuu hawa wa Wilaya. Kusiwe na kisingizio chochote, kama kuna sababu basi Jumanne mchakato huu ukamilike ili Jumatano waanze kazi mara moja.Waende wakaripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwanza kisha baadaye warudi kwa ajili ya utaratibu wa kuhama. Wakuu wa Mikoa wote warudi kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya kuwaapisha Wakuu Wilaya wamechelewa sana basi wafanye Jumanne,” amesema Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, wakuu walioteuliwa jana ni 139 kati yao 56 wapya na 83 wamebaki. 

Waziri amefafanua kwamba waliobaki 83 kati 26 wamebakishwa kwenye vituo vyao huku wengine wakihamishwa katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha utendaji nchini.

"Tunampongeza Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa Wakuu wa Wilaya. Uchambuzi wa awali unaonyesha kati ya hao wapya ni 56, wa zamani ni 83. Jumla 139. Wanaume ni 95, Wanawake ni 44 sawa na asilimia 31.6. Tunamshukuru Rais kwa kuongeza idadi ya wanawake katika Uongozi,"amesema Waziri Ummy.

Post a Comment

0 Comments