Uongozi wa Klabu ya Dodoma Jiji FC umesema kuwa, mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara mzunguko wa nane dhidi ya Tanzania Prisons FC utachezwa kwenye Uwanja wa Samora uliopo Manispaa ya Iringa Oktoba 26,2020 (Jumatatu), badala ya Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kama ilivyopangwa awali, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Dodoma Jiji FC, Ramadhani H.Juma mabadiliko hayo yanafuatia Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuwa na matumizi mengine ya tarehe ya mchezo. "Mchezo utachezwa saa 10:00 jioni na kiingilio ni shilingi elfu tatu (3,000) tu," amefafanua Afisa Habari wa Dodoma Jiji FC, Ramadhani H.Juma.