Waziri Mchengerwa awarejeshea tabasamu wanavijiji waliopoteza makazi yao kwa moto Rufiji

Na Mwandishi Wetu, Rufiji

Waziriiri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji ametoa msaada wa mabati 800 kwa wahanga wa ajali ya moto katika Kijiji cha Nyamwage wilayani Rufiji ambapo kaya 19 zimekosa makazi baada ya moto kuteketeza nyumba zao Agosti 29, 2021.
Waziri Mchengerwa ametoa msaada huo katika Kijiji cha Nyamwage alipozitembelea familia zilizoathirika na ajali hiyo ya moto kwa lengo la kuzifariji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji akishuhudia uharibifu wa ajali ya moto uliotokea hivi karibuni katika Kijiji cha Nyamwage wilayani Rufiji alipoenda kutoa pole na kukabidhi msaada wa mabati, chakula, magodoro, mavazi na vifaa vya shule.

Mhe. Mchengerwa amesema, ameamua kutoa msaada wa mabati ili kuwawezesha wahanga kuachana na nyumba za nyasi, ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari ya kupunguza athari zinazotokana na moto.

Kwa kuzingatia umuhimu wa elimu, Mhe. Mchengerwa amesema, mara baada ya ajali hiyo ya moto kutokea Serikali iliamua kuchukua hatua za haraka kwa kuwapatia sare za shule watoto 20 pamoja na madaftari na penseli ili watoto hao waendelee kupata elimu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji akitoa msaada wa chakula kwa mmoja wa wahanga wa ajali ya moto wa Kijiji cha Nyamwage Wilayani Rufiji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji akikagua nyumba zilizoathirika na ajali ya moto hivi karibuni Kijiji cha Nyamwage Wilayani Rufiji alipoenda kutoa pole na kukabidhi msaada wa mabati, chakula, magodoro, mavazi na vifaa vya shule.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji akizungumza leo na wahanga wa ajali ya moto na wananchi wa Kijiji cha Nyamwage Wilayani Rufiji mara baada ya kuwakabidhi wahanga hao msaada wa mabati, chakula, magodoro, mavazi na vifaa vya shule.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji akitoa msaada wa bati kwa mmoja wa wahanga wa ajali ya moto wa Kijiji cha Nyamwage Wilayani Rufiji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji akitoa msaada wa godoro kwa mmoja wa wahanga wa ajali ya moto wa Kijiji cha Nyamwage Wilayani Rufiji.
Baadhi ya misaada iliyokabidhiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo kwa wahanga wa ajali ya moto uliotokea hivi karibuni katika Kijiji cha Nyamwage Wilayani Rufiji.
Sanjari na hilo, Mhe. Mchengerwa kwa niaba ya Wadau wa Maendeleo Kampuni ya Lake Oil amekabidhi msaada wa chakula, magodoro, mavazi na vifaa vya shule kwa wahanga wa ajali hiyo ya moto.

Mmoja wa waathirika wa ajali hiyo ya moto, Bi. Zainabu Kapilima ameshukuru kwa kitendo cha watoto wake watatu kupatiwa msaada wa sare za shule na madaftari.

Naye, Bw. Abdallah Sango amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kuwapatia msaada wa mabati yatakazowawezesha kujenga nyumba bora na kutoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwasaidia tangu waathirike na ajali ya moto.

Akizungumza kwa niaba ya wahanga na wakazi wa Kijiji cha Nyamwage, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Mhe. Juma Ligomba amemshukuru Mhe. Mchengerwa kwa kutoa msaada wa bati ambao utaboresha makazi ya wanakijiji hao baada ya kuathiriwa na ajali ya moto kutokana na idadi kubwa ya nyumba zao kuwa za nyasi.

Mhe. Mchengerwa ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza na kutoa misaada kwa wahanga wa ajali hiyo ili waweze kurejea katika hali yao ya kawaida na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news