NA GODFREY NNKO
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limetoa taarifa kuwa mikoa 11 ya Tanzania itakosa umeme kwa saa 12, siku ya Novemba 15, mwaka huu kutokana na matengenezo yanayofanywa na shirika hilo katika njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Hata hivyo, TANESCO imewaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza. "Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa dawati la dharura la wilaya kwa msaada zaidi au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu:+255 222 194 400 na +255 768 985 100,"imefafanua taarifa hiyo.