Wakulima Nzega waonesha utayari kufanikisha ujenzi na ukarabati wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji Idudumo

NA MWANDISHI MAALUM

WAKULIMA katika Halmashauri ya mji wa Nzega mkoani Tabora, wameonesha kuwa tayari na kutoa ushikiano kwa ujenzi na ukarabati wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji Idudumo unaofadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100.
Wa pili kutoka kulia, Meneja Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji Idudumo, Bw. Juma Kibori akiwaonesha wawakilishi wa viongozi wa Halmashauri ya Nzega mji na wataalam ramani ya ujenzi na ukarabati wa neo la mradi.

Wakiongea kwa nyakati tofauti katika makabidhiano ya eneo la kazi katika skimu hiyo, Bw. Pascal Maganga ambaye ni mkulima wa zao la mpunga katika skimu hiyo amesema, ujenzi na ukarabati wa miundombi katika skimu hiyo utasaidia wakulima kulima zaidi ya mara moja katika misimu tofauti ya mvua, tofauti na sasa ambapo ukosekanaji wa miundombinu unapelekea mashamba kujaa maji na kutokulima kwa wakati na kuweza kuleta madhara kwa mazao.

“Ninaamini kuwa baada ya ujenzi na maboresho haya, kwa heka awali mkulima kama alikuwa anapata gunia 30 ila baada ya maboresho haya tutavuna zaidi,"amesema Mkulima huyo.
Mhandisi Mwinchuma Tengeneza (kulia) akimkabidhi kabrasha la eneo la kazi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu, katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Idudumo mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Explicit Main Constructors Ltd, Bw. Basil Clement (kushoto).
Akiongea wakati wa makabithiano hayo, Meneja mradi huo, Mhandisi Juma Kibori kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji amesema, eneo la skmu hiyo ya kilimo cha umwagiliaji yenye ukubwa hekta 300, na kujikita zaidi katika kilimo cha mpunga lenye chanzo chake cha maji ya Bwawa la Idudumo, lilikuwa likitumia njia za asili na sasa itajengewa mfereji mkubwa wa kupeleka maji mashambani wenye urefu wa mita 1500, vigawa maji sita, makaravati matano na mifereji ya upili yenye urefu wa mita zaidi ya mia sita.

Ameendelea kusema kuwa, awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi na ukarabati wa skimu hiyo utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700, unaotegemea kuchukua miezi nane, utaboresha miundombinu na kusaidia wakulima kuwa na kilimo cha uhakika.
Sehemu ya eneo la Bwawa la Idudumo, ambalo litafanyiwa ukarabati katika awamu nyingine ya mradi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news