Sheria ya Ushiriki na Ushirikishwaji Watanzania katika Sekta ya Madini italeta matokeo chanya-Kamishina

NA TITO MSELEM-WM

IMEELEZWA kuwa, endapo Sheria ya Ushiriki na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini itasimamiwa vizuri itawezesha kufikiwa lengo la kufikia mchango wa asilimia 10 katika pato la Taifa.
Kamishina wa Tume ya Madini, Janet Lekashingi ameyasema hayo wakati akifunga Kikao cha Chemba ya Migodi (Tanzania Chambers of Mine) na Maafisa wa Serikali kilichofanyika leo Juni 22, 2022 jijini Dodoma.

Kikao hicho kililenga kujadili juu ya utekelezaji wa Kanuni za Ushiriki na Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content), namna ya kusimamia Kanuni ya Usalama mahala pa kazi na utunzaji wa Mazingira.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Kamshna wa Tume ya Madini Janet Lekashingo amesema kuwa, vikao vya ushirikishwaji wa wadau ni muhimu kufanyika mara kwa mara, ambapo amesema huo ni mwanzo mzuri ili kupata urahisi wa kufanya biashara nchini ya madini nchini.

Kamshna Lekashingo ameshukuru kuwepo kwa vikao vya ushirikishwaji wa wadau wa Sekta ya Madini ambapo vinajadili mambo mbalimbali ya kueleimisha na kushauriana juu ya uwekezaji katika Sekta ya Madini.

"Tuendelee kuelimishana na kujadili vizuri kipengele kwa kipengele juu ya mada zilizowasilishwa leo, tumechukua changamoto zote tunaenda kuzifanyia kazi," amesema Lekashingo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Filbert Rweyemamu amesema kuwa, juhudi kwenye kuinua Sekta ya Madini inahitajika ili kuongeza thaman na ubora kwenye Sekta hiyo.

Katibu Mtendaji wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Benjamin Mchwampaka amesema vikao kama hivyo ni vyema vikafanyika mara kwa mara kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kujadili agenda mbalimbali kuhusu Sekta ya Madini ili kupata uelewa wa pamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news