WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTANGAZA UTALII WA UTAMADUNI NA MALIKALE

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Wizara ya Maliasili na Utalii iko tayari kutoa ushirikiano kwa wadau wanaofanya jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuandaa matamasha ya kutangaza utalii wa utamaduni na malikale.
Ameyasema hayo leo Juni 13, 2022 ofisini kwake jijini Dodoma alipokutana na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival litakalofanyika kuanzia tarehe 13 mwezi Agosti 2022 na kumalizika 15 mwezi Agosti 2022 katika Kata ya Kipatimo Kijiji cha Nandete Wilaya ya Kilwa.
Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya “Majimaji Tujiandae Kuhesabiwa ”litahusisha mashindano ya mbio, mashindano ya mpira wa miguu na mashindano ya ngoma za asili ambapo washindi watapewa zawadi mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news