Timu ya Iran yagoma kuimba wimbo wa Taifa Kombe la Dunia

NA DIRAMAKINI

WACHEZAJI wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hawakuweza kuimba wimbo wao wa taifa wakati wa mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia dhidi ya Uingereza leo Jumatatu.
Wachezaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakisikiliza wimbo wa taifa kabla ya mechi ya Kundi B ya Kombe la Dunia la Qatar 2022 kati ya Uingereza na Iran kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa mjini Doha leo Novemba 21, 2022. (Picha na FADEL SENNA/AFP).

Uamuzi huo wameufikia kama njia ya kuunga mkono waandamanaji wanaoipinga serikali katika nchi yao. Kabla ya mchezo huo nchini Qatar, nahodha Alireza Jahanbakhsh alisema timu hiyo itaamua kwa pamoja kukataa au kutoimba wimbo huo ili kuonesha mshikamano kwa maandamano ambayo yametikisa utawala nchini Iran.
 
Wachezaji wa Iran walisimama kwa jazba na nyuso zenye huzuni huku wimbo wao ukipigwa kuzunguka Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa mjini Doha.

Iran imetikiswa na miezi miwili ya maandamano ya nchi nzima tangu kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 katika kizuizi cha polisi kwa kukiuka maadili mnamo Septemba 16.

Amini, Mirani mwenye umri wa miaka 22 na mwenye asili ya Kikurdi, alifariki siku tatu baada ya kukamatwa mjini Tehran kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi ya Jamhuri ya Kiislamu ya wanawake, ambayo ni pamoja na uvaaji wa hijabu.

Baadhi ya wanariadha wa Iran wamechagua kutoimba wimbo wa taifa au kusherehekea ushindi wao ili kuunga mkono waandamanaji.

Jahanbakhsh, ambaye aliwahi kuchezea klabu ya Brighton ya Uingereza, alikasirishwa wiki iliyopita na swali la mwandishi wa habari wa Uingereza kuhusu suala la wimbo wa taifa huku akimtaka kuacha kumpangia maisha.

Tangu kifo cha Amini kimesababisha karibu watu 400 kuuawa, kulingana na kundi la utetezi wa Haki za Kibinadamu la Iran huko Oslo.

Hali hiyo ya leo,imesababisha maswali iwapo timu hiyo inawakilisha Iran au utawala ambao umetawala kwa mkono wa chuma tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.(Mashirika)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news