Tanzania kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Mtandao wa Chakula AFRIKA 2023

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Kilimo utakaohusisha Viongozi, watu mashuhuri na wadau wapya 3,000.

Uamuzi huo umetangazwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Hailemariam Dessalegn katika Jukwaa la Mtandao wa Chakula Afrika (AGRF) nchini Marekani.

Rais Samia amesema anatarajia mkutano huo utaendeleza uimarishaji wa mifumo ya chakula na kilimo katika vipaumbele vya Serikali, kupeana taarifa na kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya mifumo imara ya chakula.

Pia Rais Samia amesema wadau mbalimbali watakaohudhuria wataweza kujadili namna ya kuimarisha biashara miongoni mwa miji mbalimbali ili kuchangia usalama wa chakula, ukuaji na uvumilivu.

Mbali na hayo lengo lingine ni kushawishi nchi zote juu ya ajira kwa vijana ambapo kila nchi barani Afrika itaweka wazi mikakati yake ya malengo ya ajira hizo na namna ya kufanikisha.

Katika kuimarisha shughuli za kilimo serikali ya Tanzania imeongeza bajeti yake karibu mara nne katika sekta hiyo kutoka dola za Kimarekani milioni 126.7 kwa mwaka 2021/2022 hadi dola milioni 411.2 mwaka 2022/2023.

Rais Samia amewasili nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa Wakuu wa Nchi wa Afrika na Marekani utakaohusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na mikutano mengine ya kimkakati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news