Waziri Simbachawene akemea uvuvi haramu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene ametoa rai kwa wananchi wa Mtera kuacha kutumia nyavu haramu katika shughuli zao za uvuvi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata ya Mtera.

Wito huo ameutoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene katika Mkutano wa hadhara aliofanya kata ya Mtera jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

“Msitumie nyavu za timba; ambazo zina sumu, ambazo zinauwa mazalia ya samaki na hata kwa mtumiaji wa samaki, waliovuliwa kwa nyavu hizo anaathirika.”

Bwawa linashindwa kuwa endelevu kwa sababu hakuna shughuli za uvuvi zinazoendelea kutokana na kukosekana kwa samaki.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua mradi wa ujenzi wa josho katika kijiji cha Mtera.

“Afisa Uvuvi wa Halmashauiri ya wilaya ya Mpwapwa kushirikiana na Maafisa uvuvi katika maeneo yanayozunguka bwawa la mtera muandae andiko ambalo litasaidia kuja na mkakati wa Uvuvi endelevu katika bwawa la Mtera,” alisema Waziri Simbachawene.

Hii itasaidia kutengeneza vikundi vya wavuvi vitakavyopewa uwezeshaji, ili viweze kupita kwa wavuvi wenzao kuwaelimisha juu ya athari zinazotokea kutokana na wavuvi kutumia nyavu haramu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akimkabidhi baiskeli ya kutembelea Bw. Ayubu Makaburi kwa ajili ya Mwanae Mwenye Ulemavu Yusuphu Ayubu.

Naye afisa Uvuvi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bw. Fransisco Mwanga amesema uvuvi wa kutumia nyavu haramu aina ya timba ni hatari, madhara yake inapogusana na samaki ni kushindwa kuzaliana.

Elimu imetolewa kwa wavuvi na wakati mwingine kupigwa faini lakini bado wameendelea na uvuvi haramu uliosababisha samaki kutozaliana”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akimkabidhi baiskeli ya kutembelea Bw. Ayubu Makaburi kwa ajili ya Mwanae Mwenye Ulemavu Yusuphu Ayubu.

“Akizungumzia tatizo la uvuvi haramu Bwn. Hussein Mkwizu amesema swala hilo linapaswa kuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao vya maendeleo vya kijiji ili kuweza kujenga uelewa wa pamoja kwa wananchi.”

“Lazima kuwe na kikosi kazi kitakachohusisha wabunge wa Majimbo yote yanazonguka bwala la Mtera kitakachojikita katika kuelimisha umma.”

Hakuna kambi ambayo imezunguka bwawa la Mtera ambayo haijapitia hiii shida, sasa hivi kila mtu anafikiria namna tatizo hili linavyoweza kutatuliwa na lisijiruide

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news