Rais Dkt.Mwinyi awakaribisha wawekezaji kutoka Ujerumani

BERLIN-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani tarehe 20 Juni 2023 jijini Berlin. 
Mkutano huo umejadili fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana Zanzibar ikiwemo sekta ya uchumi wa buluu, maji safi na salama, umeme, elimu na vyuo vya mafunzo ya amali, tehama, viwanda na usarifu wa mazao ya kilimo na sekta ya afya.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa wote wanakaribishwa na Serikali ipo tayari kuwapokea na inawahakikishia usalama wa uwekezaji na biashara zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news