Orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili TFS-Shamba la Miti Saohill

IRINGA-Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Saohill kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) anapenda kuwataarifu waombaji wote walioomba kazi kuwa, usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia Septemba 14, 2023 ili kuwapatia ajira za mikataba waombaji kazi watakaokuwa wamefaulu usaili huo.

Hayo ni kwa mujibu wa tangazo lenye Kumb.Na.TFS.SHL/C.233/242/01/109 lililotolewa Septemba 5, 2023 na Mhifadhi Mkuu-Shamba la Miti Saohill lililopo Mafinga mkoani Iringa.

Kwa mujibu wa tangazao hilo, wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo;

1:Usaili utafanyika kuanzia Septemba 14, 2023 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu ambapo usaili huu utafanyika umeainishwa kwa kila kada.

2:Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi, kiwe cha uraia, mpiga kura, leseni au hati ya kusafiria.

3:Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne, sita, stashahada, astashahada au shahada kutegemea na sifa ya mwombaji.

4:Testimonials, result slip hazitakubaliwa.

5:Kila msailiwa anatajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
6:Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo.










Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news