NA DIRAMAKINI
SIKU chache baada ya Klabu ya Yanga kuishushia Simba SC karamu ya mabao jijini Dar es Salaam, Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba wa Kocha Mkuu wa Kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Gancalves Do Carmo (Robetinho).
Pia, klabu hiyo imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.
Katika
mtanange huo, Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam ilijikuta katika
wakati mgumu kupitia Derby ya Kariakoo baada ya kupoteza kwa mabao 5-1.
Aidha, kupitia Derby hiyo, kikosi cha Yanga kilipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Kennedy Musonda kwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Yao Attohoula.
Kibu Denis aliwapatia Simba SC bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya tisa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Said Ntibazonkiza.
Max Nzengeli aliwapatia Yanga bao la pili dakika ya 64 kwa shuti kali la chini chini baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu wa Kati.
Aziz Ki aliwapatia Yanga bao la tatu dakika ya 72 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clement Mzize.
Nzengeli aliwapatia Yanga bao la nne dakika ya 77 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi ya Mzize. Bao la tano kwa klabu ya Yanga lilipelekwa nyavuni na Pacome dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti.