Tanzania inao uwezo wa kuzalisha nondo na mabati yenye ubora kwa soko la ndani na nje

DAR ES SALAAM-Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) alitoa wito kwa Watanzania kuacha kununua bidhaa zinazotoka nje ya nchi Ilihali zinazalishwa nchini na kwa viwango vyenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.
Ameyasema hayo Januari 6,2024 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea Viwanda vya Motisun (IMMI Steel) vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo bati, nondo, plastiki, juisi na rangi.

Aidha, Dkt. Kijaji pia alosema vipo viwanda nchini vinavyozalisha bidhaa zenye ubora unaostahiki na kwamba Watanzania waache kukimbilia nje ya nchi,badala yake wanunue bidhaa zinazozalishwa nchini.

"Tanzania ina viwanda vinavyotengeneza bidhaa nzuri zisizo na mashaka, bidhaa hizo zina viwango vyote vinavyotakiwa na Taasisi za ukaguzi," amesema Dkt.Kijaji.
Aidha, aliongeza kuwa wakati Taifa likielekea kwenye Sheria ya Fedha ya mwaka 2024 ni vyema kuona namna ya kulinda viwanda kwa manufaa ya Watanzania.

Vile vile aliwashauri wenye viwanda kuwa wavumilvu kwenye changamoto ya umeme na kwamba ni kwa kipindi kifupi na ifikapo Februari 2024 kama ilivyoahidiwa na Rais Samia Suluhu Hassan suala hilo litafikia mwisho.

Alisema, Tanzania inao uwezo wa kuzalisha bidhaa inayokidhi viwango vya juu kabisa ambapo ni wakati sasa wa kuieleza Dunia juu ya bidhaa hizo ambazo zinakidhi mahitaji ya soko.
Wakati huo huo,Dkt. Kijaji alitumia muda huo kuwahamasisha wenye viwanda hao kujipanga kupeleka bidhaa zao katika masoko mengi nje ya nchi ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)na Eneo huru la Biashara Afrika (AfCFTA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news