Rais Dkt.Mwinyi awapa taarifa njema wananchi kuhusu chakula, awajulia hali wazee

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali itapunguza gharama za vyakula nchini.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo Februari 23,2024 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Msikiti wa Mubarak Bububu Kihinani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema, atatoa taarifa muda mfupi ujao katika kukabiliana na hali ya upandaji wa gharama za vyakula ili kuwapunguzia mzigo wananchi.

Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza waumini kutenda mema kwa kudumisha amani na kuwasaidia makundi ya wasiojiweza katika kuelekea kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewatembelea wazee na kuwajulia hali akiwemo Bi. Mwapombe Hiyari Mtoro wa Chuini, Mzee Daud Seleman Ali wa Fuoni Migombani na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Jang'ombe, Mzee Ramadhan Nzori.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news