Serikali kujenga Chuo cha Ufundi VETA Liganga

RUVUMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amesema Serikali imefanya maboresho makubwa katika sekta ya elimu katika kipindi cha miaka mitatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiongozana na wenyeviti wa mashina wakikagua mradi wa ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Maposeni katika Halmashauri ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipoongozana na Wenyeviti wa Mashina wa CCM katika Kata ya Parangu, Mpandangido, Kilagano na Maposeni kujionea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi kwenye ujenzi wa miundombinu ya mambweni na madarasa uliofanyika katika Shule ya Sekondari Maposeni na Mtopesi tarehe 28 Februari, 2024 katika Halmashauri ya Songea mkoani Ruvuma.
Waziri amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kupunguzia wananchi hadha ya kuchangishana michango kwa ajili ya ujenzi.

Katika Shule ya Sekondari Maposeni kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 40, ambapo kuna madarasa ambayo ujenzi umekamilika na mengine yako mbioni kujengwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza na mabalozi wa Kata ya Mpandangido, Peramiho, Parangu, Maposeni na Kilagano katika Halmashauri ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

"Hivyo basi jamii ina wajibu wa kumlinda mtoto wa kike na kumlinda mtoto wa kiume kwa kuwapatia elimu bora itakayosaidia kujenga jamii yenye weledi," alisema.

Ameongeza kuwa, zawadi nyingine aliyotupatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha anafuta ada na kusaidia watoto wengi kwenda shule.

Kutokana na ongezeko la wanafunzi, tunahitaji kuongeza miundombinu ya elimu kwa ajili ya vijana wetu.

"Serikali inaandaa mitaala mpya ambayo itasaidia kuwapa elimu ya ufundi vijana wetu waweze kupata ujuzi," alibainisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiwa katika pamoja na wenyeviti wa mashina katika Shule ya Sekondari Maposeni Halmashauri ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

Sambamba na hilo Halmashauri yetu ya Songea Vijijini, serikali itajenga chuo kikubwa cha Ufundi cha VETA katika Kata ya Liganga ili kuwezesha vijan kupata elimu ya ujuzi katika chuo hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Vijijini, Mhe. Menace Komba amesema tayari wameshaanza utaratibu wa kuomba wizara ya elimu ili kupata kibali cha kubomoa majengo ya zamani ya shule ya sekondari Maposeni na Mpitimbi ili kujenga Madarasa mapya.

"Uamuzi huo umeafikiwa na Halmashauri ya Songea Vijijini ili kuipatia shule ya sekondari Maposeni pamoja na Mpitimbi muonekano mzuri na wakuvutia,"alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiwa katika pamoja na Wenyeviti wa mashina katika shule ya sekondari Maposeni Halmashauri ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

Awali,Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mwalimu Dismass Nchimbi akizungumza mbele ya ujumbe wa wenyeviti wa Mashina alisema serikali imefanya mambo mengi katika shule ya sekondari Maposeni.

"Tumepata mradi wa ujenzi wa Mambweni 2, na Madarasa 4 na vyoo matundu 10 mradi unaofadhiliwa na Barick katika Jimbo la Peramiho, " alisema.

Serikali kwa kupitia Mbunge wa Peramiho amesaidia pia ujenzi wa jengo jipya la utawala ambalo limegharimu kiasi cha shilingi million 74 na ujenzi wake umefikia kwenye lenta

Akitoa neno la shukrani Mwanafunzi, Ahad Antony Bugari umeshukuru serikali kwa kuimarisha Miundo Mbinu ya elimu katika Shule ya Sekondari Maposeni.
Amemshukuru walimu wa Maposeni kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Miundo Mbinu ya elimu katika sekondari ya Maposeni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news