Dkt.Tulia ahimiza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kulinda amani duniani

GENEVA-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wanachama wa Umoja huo kudumisha misingi ya IPU ikiwemo kuendeleza amani na usalama, kulinda misingi ya demokrasia, kuchagiza Mabunge jumuishi, kulinda usawa wa kijinsia na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Dkt. Tulia ameyasema hayo wakati akifunga rasmi Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Geneva (CICG), nchini Uswisi tarehe 27 Machi, 2024.

Aidha, amesisitiza Viongozi wa Mabunge wanachama kuona umuhimu wa kutoa taarifa za utekelezaji ndani ya Mabunge yao juu ya maazimio ya Mikutano Mikuu yanayopitishwa ili kuleta matokea chanya kwa jamii wanayoiwakilisha.
Vilevile amesema kuwa, IPU ni sehemu pekee ambayo Mabunge yanakutana kwa pamoja kupitisha maazimio yanayoihusu dunia na hivyo ni muhimu kwa Maspika wa Mabunge wanachama kuhudhuria Mikutano ya Umoja huo.

Mkutano wa 148 umehitimishwa rasmi leo huku ukiwa umehudhuriwa na takribani misafara ya Mabunge zaidi ya 145.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news