Rais Dkt.Samia kuanza ziara ya siku tatu nchini Angola

DODOMA-Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Angola, kufuatia mwaliko wa Rais João Manuel Gonçalves Lourenço wa nchi hiyo.
Ziara hiyo inalenga kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Angola.

Akiwa nchini Angola, Rais Samia atapata fursa ya kufanya mazungumzo ya uwili na mwenyeji wake Rais Lourenço, kuhutubia Bunge la Angola, kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Mwasisi wa Taifa hilo Hayati António Agostinho Neto, pamoja na kutembelea kiwanda cha mafuta cha Luanda.

Ziara hiyo pia itashuhudia uwekaji saini wa Hati za Makubaliano (MOU) katika masuala yanayolenga kufungua fursa za biashara na uwekezaji na jitihada za kuimarisha ulinzi na usalama.

Uhusiano wa Tanzania na Angola uliasisiwa na waasisi wa mataifa hayo ambao ni Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati António Agostinho Neto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news