Mtendaji wa Kata ya Kainam wilayani Mbulu hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi

MANYARA-Leo Julai 17,2025 Mahakama ya Wilaya ya Mbulu katika shauri la uhujumu uchumi la ECC.No.13987/2025 imemtia hatiani mshtakiwa Mtendaji wa Kata ya Kainam,Bw. Eliwangu Fadhili Mkumbwa kwa kosa la ufujaji na ubadhirifu wa fedha za mradi wa Kituo cha Afya Kainam alizozitumia kwa manufaa yake binafsi.
Kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 28(1)cha PCCA Cap 329 R: E 2023 vikisomwa pamoja na aya ya 21 katika jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Kudhibiti Uhujumu Uchumi na Makosa ya Kupanga Sura 200 R: E 2023.

Kesi hii imeendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) wilayani humo,Bi.Neema Gembe.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Wilaya ya Mbulu,Mheshimiwa Vitus Kapugi amemtia hatiani mshtakiwa baada ya mshtakiwa huyo kufanya makubaliano (plea bargaining agreement) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Mshtakiwa amepewa adhabu ya kulipa faini ya kiasi cha shilingi 100,000 au akishindwa kutumikia kifungo cha gerezani kwa muda wa miezi sita pamoja kurejesha fedha alizozifanyia ubadhirifu kiasi cha shilingi 3,129,000 kwa muhusika.

Hadi hukumu inasomwa mshtakiwa amefanikiwa kurejesha kiasi cha shilingi 1,560,000 katika akaunti ya Kainam Community Account (muhusika) iliyopo Benki ya NMB na kiasi kilichobaki atatakiwa kurejesha kabla au ndani ya miezi sita kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa plea bargaining.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news