Profesa Shemdoe awataka waliokwenda kusherehekea Krismasi vijijini kununua bidhaa za wenyeji

NA JAMES MWANAMYOTO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewahimiza wananchi waliosafiri kutoka mijini kwenda vijijini, kuhakikisha wananunua bidhaa huko huko vijijini ili kuleta tabasamu na kuongeza mzunguko wa fedha vijijini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe akitoa salamu za Krismass kwa watanzania, mara baada ya ziara yake ya kikazi aliyoifanya kwenye Soko la Kariakoo jijini Dar Es Salaam.

Prof. Shemdoe ametoa wito huo katika salaam zake za Krismasi alizotoa Disemba 24, 2025, mara baada ya ziara yake ya kikazi aliyoifanya kwenye Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

"Ndugu Watanzania wenzangu ambao tumefanikiwa kwenda kusherehekea Sikukuu ya Noel vijijini kwetu, tuhakikishe tunanunua bidhaa zinazopatikana vijijini huko huko kwa wenyeji wetu, ili tuwaachie tabasamu na kuunga mkono azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuinua kipato cha Watanzania,” amesisitiza Prof. Shemdoe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news