Ubunifu katika mazingira ya kazi si anasa ni tija-Mbibo

SIMIYU-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amesisitiza kuwa ili watumishi wa umma waweze kuongeza ufanisi kazini na kuwajibijika wanapaswa kuwa wabunifu katika mazingira yao ya kazi ili kuendana na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia na kimazingira na kwamba ubunifu katika mazingira ya kazi sio anasa bali ni kuongeza tija.
Alisema hayo, Desemba 29, 2025 wakati ziara ya kikazi kukagua shughuli za madini katika Mkoa wa Simiyu na kutaka watumishi wa Tume ya Madini mkoani humo kuweka msisitizo mkubwa kwenye ubunifu wa mazingira ya kazi kama nyenzo ya kuongeza Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali.

Mbibo alieleza kuwa dunia inabadilika kwa kasi kubwa kupitia teknolojia na mifumo mipya ya utendaji, hivyo watumishi wa umma, hususan katika Sekta ya Madini, hivyo hawana budi kubadilika sambamba na mabadiliko hayo kwa kuimarisha ubunifu, weledi na uwajibikaji kazini.
“Ubunifu katika mazingira ya kazi si anasa, bali ni tija na hitaji la msingi katika kuongeza ufanisi, tija na hatimaye kufikia malengo ya Serikali ikiwemo makusanyo ya maduhuli,” alisisitiza Mbibo, huku akiipongeza Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Simiyu kwa kuendelea kufikia lengo la makusanyo ya maduhuli kila mwaka pamoja na kuonesha mshikamano kazini.

Aidha, Mbibo alipongeza mahusiano mazuri ya kikazi yaliyopo kati ya watumishi wa ofisi hiyo na wadau wa Sekta ya Madini katika mkoa huo, akieleza kuwa ushirikiano huo ni nguzo muhimu katika kusimamia shughuli za madini kwa uwazi, nidhamu na kwa manufaa ya Taifa.
Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Simiyu Mhandisi Mayigi Makolobela, libainisha kuwa, katika mwaka wa 2025/2026 Mkoa huo umepewa lengo la kukusanya shilingi bilioni 4.76, ambapo hadi kufikia tarehe 24 Disemba 2025, jumla ya shilingi bilioni 2.32 zimekusanywa sawa na 49.32% ya lengo la mwaka na kwamba matumini ya kufikia lengo kufikia mwisho wa Mwaka wa Fedha ni makubwa.

Watumishi wa Ofisi ya RMO Simiyu nao hawakusita kuonyesha shukrani zao, wakieleza kuwa ujio wa mara kwa mara wa viongozi wa juu Serikali na Kkisekta huwasaifia kuzingatia misingi muhimu ya kiutendaji, huwapa mwelekeo sahihi kupitia maelekezo yao na kuwaandaa kukabiliana na changamoto mpya zinazokuja na kasi ya maendeleo ya teknolojia duniani.
Ziara hiyo imeelezwa kuwa chanzo cha motisha mpya, ikitarajiwa kuimarisha zaidi ubunifu kazini, ushirikiano na hatimaye kuongeza mchango wa sekta ya madini katika makusanyo ya Serikali na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news