Serikali kujenga vituo 698 vya Polisi nchini

ZANZIBAR-Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema, Serikali imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 79 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi 698 nchini, ikiwa ni mkakati wa kuimarisha usalama wa raia na mali zao.​
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya Vituo vya Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar,Mhe. Ayoub Mahmoud amebainisha kuwa uamuzi huo umekuja baada ya Serikali kuona kuna uhitaji wa kusogeza huduma za Kipolisi karibu na wananchi zaidi​.
Naibu Waziri ameeleza kuwa ingawa nchi nzima inahitaji jumla ya Vituo vya Polisi 3,900, Serikali imeanza na kipaumbele cha kujenga vituo 698 katika maeneo yenye changamoto zaidi.
Kadhalika, amebainisha kuwa Mpango huo wa Shilingi Bilioni 79 unatekelezwa katika hatua tatu, ​hatua ya Kwanza ni Vituo 196, ​hatua ya Pili ni Vituo 213 na ​hatua ya Tatu ni Vituo 212 ambapo ameeleza kuwa ​Vyanzo vya fedha hizo zitapatikana kupitia bajeti kuu ya Serikali na matumizi ya Mfuko wa Tuzo na Tozo wa Jeshi la Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here