UNFPA na Ubalozi wa Tanzania Comoro katika mazungumzo ya ushirikiano

MORONI-Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Bi. Josiane Yaguibou, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu kwa nchi za Comoro, Mauritius, Seychelles na Madagascar.Katika mazungumzo yao wamezungumzia majukumu ya UNFPA kama miongoni mwa waratibu wa Sensa ya Watu nchini Comoro itakayofanyika mwakani 2027 na kuona namna Tanzania inavyoweza kushiriki kama mdau.
Balozi Yakubu alimueleza Bi.Josiane namna Tanzania ilivyoendesha kwa mafanikio makubwa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ikiwa na waangalizi wa kimataifa na vifaa vya kisasa.
Bi.Josiane aliahidi kuendeleza mawasiliano na Ubalozi ili kupata uzoefu wa Tanzania kwa mafanikio ya Sensa ya Comoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here