Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu na Afisa Mkuu wa Utawala wa Benki ya Dunia, Bw. Wencai Zhang, katika Ofisi za Benki hiyo, jijini Washington D.C nchini Marekani, wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF iliyofanyika jijini humo, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete na maafisa wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya Dunia.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















