Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu, ameshiriki Jukwaa la Tanzania na Misri la Utalii, Biashara na Uwekezaji na kueleza kuwa Tanzania imeongeza biashara ya mifugo na mazao ya mifugo katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kuwa unazingatia uwazi, ubora na uaminifu katika biashara.
Akizungumza katika jukwaa hilo (Tanzania–Egypt Tourism, Trade and Investment Forum) lililofanyika nchini Misri na kuwakutanisha wadau wa biashara, uwekezaji na utalii, Bangu amesema mfumo unaotumika kusimamia biashara ya mazao ya kilimo sasa uko tayari kuhudumia pia sekta ya mifugo.Akifafanua ufanisi wa matumizi ya mfumo huo katika moja ya mijadala iliyokuwepo kwenye jukwaa hilo, Bangu amesema wamefanya kikao kifupi na ujumbe wa Misri ambao wameonesha nia kubwa ya kufanya biashara ya mifugo na bidhaa zitokanazo na mifugo kutoka Tanzania.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






























