Tanzania Prisons FC yatozwa faini ya shilingi milioni 20 kwa imani za kishirikina uwanjani

NA GODFREY NNKO

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeitoza faini ya Shilingi milioni 20 Klabu ya Tanzania Prisons kwa kosa la wachezaji wake kufanya vitendo vilivyodaiwa kuwa ni vya kishirikina kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 29,2026 jijini Dar es Salaam na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,adhabu hiyo inatokana na tukio lililotokea kwenye Mechi Namba 226 dhidi ya Mtibwa Sugar FC iliyochezwa na kuishia kwa Prisons kushinda 2-1.
Imeeleza kuwa, wachezaji wa Prisons walipoingia uwanjani kwa mazoezi ya kupasha misuli, walizunguka uwanja mzima na walipofika kwenye vibendera walipasua mayai.

Aidha, baadaye walijikusanya katikati ya uwanja na kumwaga vimiminika vinavyodhaniwa kuwa ni ute wa mayai.

TPLB imebainisha kuwa,hilo ni kosa la kujirudia kwa Tanzania Prisons, ambapo timu hiyo ilifanya kosa linalofanana na hilo kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Bodi imeeleza kuwa adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here