Msigwa akagua maboresho Viwanja vya AFCON 2027

DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya maboresho katika uwanja wa uhuru na viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Katika ziara hiyo, Bw. Msigwa amekagua Uwanja wa Uhuru na kujionea hatua mbalimbali za maboresho yanayoendelea ikiwemo ufungwaji wa viti vya kisasa, upanuzi na ukarabati wa vyumba vya wachezaji, eneo la watu maarufu (VVIP) pamoja na sehemu maalum zitakazotumiwa na Waandishi wa Habari wakati wa mashindano hayo.

Aidha, amefanya ukaguzi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuangalia maendeleo ya marekebisho yanayofanyika katika eneo la kuchezea (pitch) pamoja na maboresho ya sehemu ya watu maarufu, hatua inayolenga kuhakikisha uwanja huo unakidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya AFCON 2027.
Aidha, ametembelea viwanja vya mazoezi vitakavyotumika katika michuano hiyo ambavyo ni Gymkhana 2, Farasi na Leaders Club, ambapo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzj yanayoendelea katika maeneo hayo.

Ziara hiyo imelenga kufuatilia kwa karibu kasi ya utekelezaji wa maandalizi ya miundombinu ya michezo, kuhakikisha maboresho yote yanakamilika kwa wakati na Tanzania inakuwa kwa mashindano hayo kwa viwango vinavyotakiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here