MARA-Mkuu wa Polisi Mkoa wa Tarime-Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jumanne Mkwama, Agosti 1, 2026, aliongoza mazoezi ya pamoja yaliyowakutanisha askari wa Jeshi la Polisi na wananchi wa Wilaya ya Tarime, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya, mshikamano na ushirikiano katika kudumisha amani na usalama.
Mazoezi hayo yaliwashirikisha askari wa Jeshi la Polisi, waendesha bodaboda, wadau mbalimbali pamoja na wananchi, ambapo washiriki walitembea kwa pamoja katika mitaa mbalimbali ya mji wa Tarime, wakionesha mshikamano na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika masuala ya ulinzi na usalama.
Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Mkurugenzi wa Mwera Foundation, Hezbon Peter Mwera, alimshukuru ACP Jumanne Mkwama kwa kuratibu na kuongoza zoezi hilo, akisema limeendelea kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.
Aidha, amelipongeza Jeshi la Polisi pamoja na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa kwa ubunifu wa kuanzisha mazoezi yanayoshirikisha jamii, huku akiomba yawe endelevu kwa kuwa yanarahisisha utoaji wa taarifa za uhalifu na kuimarisha usalama katika Mkoa wa Tarime-Rorya.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Waendesha Bodaboda, Dickson Christopher, ameishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwashirikisha wananchi katika mazoezi hayo na kuahidi kuwa waendesha bodaboda wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazolenga kuimarisha amani, usalama na maendeleo ya Mkoa wa Tarime-Rorya.

Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tarime, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Fatuma Mbwana, amesema lengo la kuwakutanisha askari wa Jeshi la Polisi na wananchi kupitia mazoezi hayo ni kuimarisha ukaribu, uhusiano mwema na ushirikiano katika kudumisha amani na usalama.
Ameongeza kuwa mazoezi ya pamoja huwapa wananchi fursa ya kuelewa kwa karibu majukumu ya Jeshi la Polisi na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika kuzuia na kupambana na uhalifu.
Mazoezi hayo ni sehemu ya juhudi za Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime-Rorya za kuendeleza dhana ya Polisi Jamii kwa kushirikiana na wananchi katika kujenga mazingira salama, kuimarisha u
