Kaya 100,000 zitaunganishwa na intaneti ndani ya miaka mitatu Zanzibar-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali inalenga kuunganisha kaya 100,000 na huduma za intaneti kupitia mfumo wa Fibre-to-the-Home ndani ya miaka mitatu, huku ikiandaa Mfumo Mkakati wa Akili Unde (AI Strategy Framework) utakaoongoza matumizi salama na yenye uwajibikaji ya teknolojia hiyo.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 29,2026 wakati akifungua Maonesho ya Teknolojia na Akili Unde (Tech and AI Expo Zanzibar 2026) katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar, sambamba na uzinduzi wa Sera ya Kidijitali ya Zanzibar 2026.
Amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejidhatiti kuendeleza mageuzi ya kidijitali kwa kuimarisha miundombinu, kuongeza matumizi ya teknolojia katika huduma za umma na uchumi, pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana, wabunifu na wawekezaji.
Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kimkakati (MoU) baina ya Wizara ya Mawasiliano,Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar na Huawei Technologies Tanzania Limited.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here