Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

DAR-Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu tarehe 18 Septemba, 2026 ametoa maagizo kwa uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhusu hatua za kuchukua ili kuongeza ufanisi na kuimarisha utendaji wa wakala huo.
Maagizo hayo yametolewa wakati wa kikao kati ya Msajili wa Hazina na uongozi wa TANROADS katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) jijini Dar es Salaam, huku ujumbe wa TANROADS ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Mhandisi Mohamed Besta.

Maagizo hayo yamelenga kuhakikisha TANROADS inaendelea kuimarisha ufanisi, uwajibikaji na tija katika utekelezaji wa majukumu yake, pamoja na kuongeza thamani ya uwekezaji wa Serikali katika miundombinu ya barabara.
OTR ina jukumu la kusimamia uwekezaji na maslahi ya Serikali katika taasisi na kampuni za umma, zikiwemo kampuni ambazo Serikali ina hisa chache. Kwa wa sasa, OTR inasimamia jumla ya taasisi na kampuni 308.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here