Rais Dkt.Mwinyi atoa pole kwa familia ya marehemu Mama Fatma Karume

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefika nyumbani kwa familia ya marehemu Mama Fatma Karume huko Mbweni, Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja leo Septemba 22, 2026 kutoa pole na rambirambi kufuatia kifo chake.
Mama Fatma Karume alikuwa mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amesaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa wanafamilia, akiwataka kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewaomba wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kuendelea kumuombea Marehemu Mama Fatma Karume, Mwenyezi Mungu amrehemu na amjaalie makaazi mema Peponi, huku akiwaombea wafiwa subira na moyo wa ustahimilivu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here