Tanzania na Misri kushirikiana katika uongezaji thamani madini ya kuzalisha mbolea

CAIRO-Pembezoni mwa Mkutano wa Madini wa Misri (Egypt Mining Forum), Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Petroli na Rasilimali Madini wa Misri,Mhe. Karim Badawi ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika uongezaji thamani madini ya kuzalisha mbolea ili kuchochea ukuaji wa uchimbaji wa madini na ukuzaji wa sekta ya kilimo.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Septemba 27, 2027 walipokutana wakati wa Mkutano wa Madini wa Misri, unaofanyika katika Hoteli ya St. Regis jijini Cairo.

Tanzania na Misri zina historia ya muda mrefu wa mashirikiano ambapo kupitia Viongozi Wakuu wa Nchi wameendelea kuimarisha uhusiano huo kwa kufanya ziara za kutembeleana kwa nyakati tofauti.
"Ni katika misingi hiyo hiyo ya Viongozi wetu Wakuu tumeweza kukutana kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kukukubaliana maeneo ya kuimarisha ushirikiano zaidi baina ya nchi zetu,"amesema Waziri Mavunde.

Kwa upande wake, Mhe. Badawi amebainisha kwamba pamoja na mengine, amevutiwa na kuipongeza Tanzania kwa namna ilivyoweka utaratibu mzuri wa kusimamia wachimbaji wadogo na kupelekea kuwa na mchango wa zaidi ya asilimia 40 ya mapato yanayokusanywa kwenye sekta ya madini.
Katika hatua nyingine, Mawaziri hao wamekubaliana kubadilishana uzoefu kupitia wataalamu hususan katika utafiti wa madini na uendelezaji wa madini ya phosphate.

Vilevile, Waziri Mavunde amebainishakuwa Tanzania ina kiwango kikubwa cha madini ya phosphate lakini bado hayajaweza kuzalishwa kwa tija na kusaidia upatikanaji wa mbolea, ambapo mpaka sasa Tanzania inakadiriwa kutumia zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 500 kuagiza mbolea kutoka nje, na kuiomba Misri iweze kusaidia katika sekta ndogo ya mbolea.
Akizungumzia hoja hiyo, Waziri Badawi ameahidi kuzingumza na wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa wa mbolea ya Phosphate ili waweze kufanya ziara nchini Tanzania kwa lengo la kuangalia fursa ya kuwekeza katika uchimbaji na uongezaji thamani madini yakiwemo ya phosphate.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here