DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Balozi Waziri Salum amekutana na kuzungumza na waajiriwa wapya wa Wizara ya Viwanda na Biashara Oktoba 12,2026 katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma.
Balozi Waziri amewataka waajiriwa hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kwa weledi ili kusaidia sekta ya viwanda na biashara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum akizungumza na waajiriwa wapya wa wizara hiyo (hawapo pichani) jijini Dodoma leo.Aidha, amewataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi na kwa ushirikiano kutoka kwenye idara zao mpaka kwa wananchi wanaowahudumia ili kuleta matokeo chanya kwa Wizara.
Tags
Ajira Mpya Serikalini
Balozi Waziri Salum
Dodoma
Habari
Waajiriwa Wapya
Wizara ya Viwanda na Biashara

