Dar: BoT kushirikiana na Benki ya Dunia kuimarisha usimamizi wa akiba ya Fedha za Kigeni kupitia ISDA na GMRA

DAR-Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo, amepokea ujumbe wa wataalamu kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Bw. George Bentley, katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Oktoba 2026.
Mazungumzo yakiendelea baina ya Naibu Gavana, Bi. Sauda Msemo na ujumbe wa wataalamu kutoka Benki ya Dunia jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huo unatarajiwa kuendesha mafunzo kuhusu matumizi ya mikataba ya kimataifa ya miamala ya kifedha, ambayo ni International Swaps and Derivatives Association (ISDA) na Global Master Repurchase Agreement (GMRA), inayotumika katika utekelezaji wa miamala mbalimbali kwenye masoko ya fedha ya kimataifa.
Mafunzo hayo yataimarisha uwezo wa Benki Kuu katika usimamizi wa akiba ya nchi ya fedha za kigeni, kuongeza ufanisi wa shughuli za masoko ya fedha, na kusaidia juhudi za kuendeleza miundombinu ya soko la fedha pamoja na usimamizi madhubuti wa hatari kwa kuzingatia viwango na mbinu bora za kimataifa.
Picha ya pamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here