El Niño: Wizara ya Maji kuwa na Timu ya Dharura kuhakikisha huduma haiyumbi

SEKTA ya Maji imejipanga kuhakikisha miundombinu ya maji haileti madhara kwa wananchi msimu wa mvua za El Niño kama ilivyotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA).
Naibu Waziri wa Maji,Mhe.Mhandisi Kundo Andrew Mathew (Mb) amesema watendaji wa mamlaka za maji hasa maabara za ubora wa maji kujipanga na kuchukua tahadhari kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma ya majisafi na salama wakati wote.

Aidha, kuwa na timu ya dharura ambayo itahusika katika kuchukua hatua za haraka za urejeshaji wa huduma ya maji pale changamoto ya ukosefu wa huduma itakapojitokeza.
"Wataalamu wetu waendelee kufanya tathmini ili kubaini maeneo ambayo yana miundombinu dhaifu ambayo inaweza kusababisha changamoto ya upatikanaji wa maji na kuchukua hatua za haraka," Mhandisi Kundo amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here