Madrid: Rais Dkt. Mwinyi atembelea makumbusho ya historia ya soka

MADRID-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelea Makumbusho ya Historia ya Magwiji wa Soka (LEGENDS: The Home of Football) pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii katika Jiji la Madrid, nchini Uhispania akiendelea na ziara yake nchini humo.
Rais Dkt. Mwinyi akiambatana na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa anayewakilisha pia Hispania, Mhe. Saidi Yakubu ametembelea makumbusho hayo leo Oktoba 11, 2026 na kujionea kumbukumbu mbalimbali za historia ya soka duniani, zikiwemo jezi na vifaa vya magwiji wa mchezo huo.

Ziara hiyo inaendana na juhudi za kuendeleza sekta ya michezo kupitia ujenzi wa miundombinu ya kisasa na kuimarisha fursa za vijana kushiriki na kuendeleza vipaji vyao Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here