DAR-Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Posta kwa kushirikiana na United Artists Of Tanzania (UAT) wanakuletea tamasha kubwa la Museum Art Explosion litakalofanyika Oktoba 30, 2026 jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo linalotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku hadi saa 4:00 usiku, litajumuisha burudani mbalimbali ikiwemo miondoko ya angani, dansi za asili na za kisasa, pamoja na burudani ya muziki kutoka kwa Malaika Band.