Miaka 20 jela pamoja na fidia kwa unyanyasaji wa kingono Mkuranga

NA DIRAMAKINI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imemhukumu, Daud Paschal Lushanga (36) mkazi wa Mlamleni wilayani Mkuranga Mkoa wa Kipolisi Rufiji kifungo cha miaka 20 jela.
Ni baada ya kupatikana na hatia ya kosa la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.

Mbali na kifungo hicho, Mahakama imemtaka kumlipa mhanga fidia ya Shilingi milioni 2 kufuatia ushahidi uliotolewa na upande wa Mashtaka uliothibitisha kosa hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kesi namba 12231/2026 tukio hilo lilidaiwa kutokea Mei 8, 2026 majira ya saa 11:30 jioni katika eneo la Kisasa ‘A’ wilayani Mkuranga.

Mshtakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha sheria, huku akimsababishia mtoto huyo maumivu makali.

Katika mwenendo wa kesi hiyo upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi sita mahakamani ili kutoa ushahidi wao kuhusu tukio hilo.

Baada ya shauri kusikilizwa hadi mwisho, Mahakama iliridhika kuwa ushahidi uliotolewa ulithibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa bila kuacha shaka, na hivyo kumtia hatiani kwa kosa lililokuwa likimkabili.

Hukumu hiyo imesomwa Oktoba 9, 2026 mbele ya Hakimu Kenedy Mrosso. Adhabu iliyotolewa inalenga kutekeleza haki kwa mhanga kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama huku ikisisitiza umuhimu wa kulinda watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kingono na kuhakikisha wanaopatikana na hatia wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here